WATANZANIA 225 HUAMBUKIZWA VIRUSI VYA UKIMWI KILA SIKU - BoomFleva
TANGAZA NASI KUPITIA NO 0756976042

Search This Blog

Wednesday, 7 March 2018

WATANZANIA 225 HUAMBUKIZWA VIRUSI VYA UKIMWI KILA SIKU

Takwimu zinaonesha kuwa Watanzania 225 huambukizwa Virusi vya Ukimwi kwa siku.

Hali hiyo inamaanisha kwamba kwa mwezi watu 6,750 huambukizwa VVU na kwa mwaka ni 81,000.

Takwimu hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko, jana Jumanne Machi 6, wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu uandaaji wa programu bora za Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi.

Amesema hali hiyo ni mbaya zaidi kwa vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24.

“Asilimia 40 ya maambukizo mapya hutokea kwa vijana wenye umri Kati ya miaka 15 hadi 24 na kati yao wengi ni wanawake.

“Hii inamaanisha kwamba katika hiyo asilimia 40 ya vijana waliopata maambukizi mapya, asilimia 80 ni wanawake,” amesema Dk. Maboko

No comments:

Post a Comment